Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya nadwa ya kielmu yenye anuani isemayo (Kuenea kwa uislamu katika bara la Afrika) katika mkoa wa Najafu.
Nadwa imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya kwa kushirikiana na kitivo cha adabu kwenye chou kikuu cha Mustanswiriyya, imehudhuriwa na wasomi wa mambo ya Afrika pamoja na wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika.
Nadwa ilikuwa na mada tano kutoka kwa wabobezi wa historia ya Afrika, wameongea mwanzo wa kuingia uislamu katika bara la Afrika nan chi za kwanza ambazo raia wake waliingia kwenye uislamu, sambamba na kueleza mchango wa taasisi za Dini katika kusambaza Dini, mada zimejikita katika kueleza uingiaji wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) katika bara la Afrika, aidha yamejadiliwa mazingira ya elimu, maadili, 0uchumi na rasilimali za Afrika.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri ameeleza kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika bara la Afrika kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, miongoni mwa ratiba za kidini, kisekula, kibinaadamu, ikiwemo uchimaji wa visima na misaada ya kibinaadamu kwa wananchi wa Afrika.
Akasisitiza kuwa nadwa hii inatokana na ushirikiano uliopo kati ya Markazi na taasisi za kisekula za Iraq, akasema wanatarajia kufanya nadwa na warsha za kielimu kwa kushirikiana na vyuo vikuu tofauti vya Iraq, akaonyesha umuhimu wa kuwapa nafasi wasomi wa mambo ya Afrika, Pamoja na kufungua milango ya maktaba ya Markazi kwa wasomi na watafiti sambamba na kuandika vitabu kwa jina la Markazi Dirasaati Afriqiyya.