Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza majina ya washindi wa shindano la kitamaduni kuhusu mazazi ya Imamu Muhammad Aljawaadi (a.s).
Sharti la kupokea zawadi mshindi anatakiwa awepo katika hafla ya kuzaliwa Imamu Muhammad Aljawaadi (a.s), itakayofanywa katika eneo la uwanja wa mlano wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumatatu (22/1/2024m) sawa na (10 Rajabu 1445h) saa moja jioni.
Iwapo mshindi atakuwa na udhuru wa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa kufika kwenye ofisi za mali (wahasibu) ndani ya muda usiozidi siku nne toka kutangazwa kwa matokeo, akiwa na kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria.