Shada za mauwa zimepamba dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Idara inayosimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imepamba dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuweka shada za maua kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Aljawaadi (a.s).

Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twaif amesema “Watumishi wa idara yetu wamepamba dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) mwezi kumi Rajabu, itakayofuatiwa na kumbukumbu ya kuzaliwa babu yake Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya upambaji imehusisha kuweka shada za mauwa yenye rangi tofauti kwa lengo la kuongeza uzuri juu ya kaburi tukufu la mwezi wa bani Hashim (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu huweka mazingira ya furaha kwa kupamba dirisha la malalo takatifu katika kumbukumbu za kuadhimisha mazazi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: