Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya shindano la (kiongozi mwema) kwa njia ya mtandao, kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).
Kiongozi wa Idara Bibi Adhraa Shami amesema “Idara imezowea kufanya harakati mbalimbali wakati wa matukio ya kidini ndani ya mwaka mzima”.
Akaongeza kuwa “Shindano linamaswali ishirini yanayo husu historia ya kiongozi wa waumini (a.s), matokeo yatatangazwa mwezi kumi na mbili Rajabu, tumeandaa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo, shindano linaendeshwa kupitia link maalum”.
Akasema “Shindano hili ni sehemu ya maadhimisho ya mazazi haya matukufu na kujenga uwelewa wa kidini katika jamii sambamba na kuendeleza fikra za mwanamke wa kiislamu”.