Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeshiriki kwenye kongamano la kitaifa la wanachuoni wa kiislamu nchini Senegal chini ya kauli mbiu isemayo (Kuishi kwa amani baina ya makundi ya kiislamu).
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Muwakilishi wa kitengo nchini Senegal na mkuu wa kituo cha Mukhtaaru Lidirasaati Alqur’aniyya wal-Islamiyya, Shekhe Mustwafa Diba, ameshiriki kwenye kongamano la kitaifa la wanachuoni wa kiislamu”.
Akaongeza kuwa “Ushiriki wa Markazi ni sehemu ya kuendeleza mawasiliano na taasisi za kielimu na kijamii katika nchi za Afrika” akasema “Aidha uwepo wa Markazi katika jamii za waafrika unaonekana kupitia miradi ya kibinaadamu na kueneza mafundisho ya Ahlulbait (a.s)”.
Katika ujumbe aliotoa kwaniaba ya Markazi Shekhe Diba amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na kujenga mapenzi na amani katika jamii, akafafanua ratiba mbalimbali zinazofanywa na Markazi katika nchi ya Senegal, ikiwemo miradi ya kibinaadamu, kielimu na Qur’ani.