Akisisitiza umuhimu wa tarjama.. Sayyid Swafi ametoa wito wa kuandika kwenye sekta tofauti.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa tarjama katika lugha zingine na kuandika katika sekta tofauti.

Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya kuadhimisha miaka kumi toka kuanzishwa kwa kituo cha kiislamu na tafiti za kimkakati, iliyofanywa katika mji wa Najafu na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya, walimu na wanafunzi wa hauza.

Sayyid Swafi akasema “Kuna kalamu nzuri inapasa kunufaika nazo na kuhisi wajibu kwa kila mtu mwenye uwezo wa kuandika na aandike, na sisi tutachukua vitabu hivyo na kuvichapisha na kuvisambaza”.

Kuhusu umuhimu wa tarjama akasema “Baadhi ya nchi wanaweza kuwa na vitu vyenye manufaa lakini visitufikie kwa lugha ya kiarabu, inaweza kuwa yameandikwa kwa lugha zingine, atakae jitolea kutafsiri sisi tukotayali kuchapisha na kusambaza”.

Akasema kuwa “Kuna haja kubwa ya kufanya hivyo, hasa kwa vijana wanaosubiri kitu cha kujikinga na njaa, ukitembelea maktaba na kufanya harakati ambayo matunda yake yataonekana katika jamii”.

Akaongeza kuwa “Markazi imeshachapisha majarida mengi na imeangalia namna wengine wanavyosoma uislamu, aidha kituo kimeingia katika swala la umagharibi na kuangalia namna wengine wanavyo soma sambamba na kunufaika na watafiti kutoka nchi za Afrika kaskazini, walipoona baadhi ya machapisho ya kituo hiki walitupigia na wakaomba machapisho yetu, tunazo nyaraka za barua tumezihifadhi zinazo onyesha namna wanavyojali harakati zetu kwa ujumla”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: