Ataba mbili tukufu Abbasiyya na Zainabiyya zimejadili njia za kushirikiana katika kuhudumia mazuwaru wa malalo zao takatifu.
Hilo limefanywa baada ya ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unao ongozwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawadi Hasanawi, kukutana na kiongozi mkuu wa Atabatu Zainabiyya Muhandisi Maazin Aali Murtadha na kujadili njia za kushirikiana katika kuhudumia mazuwaru wa malalo ya Bibi Zainabu (s.a).
Hasanawi ametembelea baadhi ya miradi ya Atabatu Zainabiyya, ukiwemo ukumbi mpya utakao funguliwa karibuni kwa lengo la kuboresha huduma kwa mazuwaru.
Mwisho wa matembezi hayo Aali Murtadha ameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na viongozi wake, kwa msaada mkubwa wanaotoa katika malalo ya Bibi Zainabu (a.s).