Ratiba ya siku ya pili katika kongamano la kiongozi wa waumini (a.s) katika mji wa Mombai nchini India inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na Ataba zingine za Iraq imeanza.
Kauli mbiu ya kongamano inasema (kiongozi wa waumini (a.s) ni Haruna wa Uimamu na shahidi siku ya Kiama), nalo ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali -a.s- kwenye msikiti wa Mukai – katika mji wa Mombai nchini India, kongamano litadumu kwa muda wa siku tatu, kwa lengo la kufundisha utamaduni wa Ahlulbait (a.s) na elimu yao.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kutoka kwa msomaji wa Atabatu Alkadhimiyya Sayyid Baaqir Ahmadi, ukafuata ujumbe wa Ataba tukufu za Iraq (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya) uliwasilishwa na rais wa ujumbe wa Atabatu Alkadhimiyya Shekhe Adi Alkadhimi.
Katika hafla hiyo chakula kimetolewa kwa wahudhuriaji miongoni mwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), sambamba na kutoa koponi za bahati nasibu ya Kwenda kutembelea Ataba za Iraq, hafla ikahitimishwa kwa kuimba Qaswida zinazoendana na tukio hilo.
Siku ya kwanza ya kongamano hilo watu wenye majina ya Ali walipewa zawadi, na kupandishwa bendera za kubba tukufu za malalo ya Iraq, sambamba na kufungua maonyesho ya vitabu yanayo husisha idara tano kutoka kwenye hizo Ataba tukufu.