Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umeweka mapambo meusi kwenye malalo ya Bibi Zainabu (a.s) katika kuomboleza kifo chake.

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya nchini Sirya, umeweka mapambo meusi ndani ya haram ya Bibi Zainabu (a.s) katika kuomboleza kifo chake.

Mjumbe wa ugeni huo Muheshimiwa Khaliil Mahadi Hanuun amesema “Ugeni wa Ataba tukufu kwa kushirikiana na viongozi wa Atabatu Zainabiyya, wamewema mapambo meusi na vitambaa vilivyo dariziwa maneno ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Wameweka vitambaa vyenye ukubwa tofauti ndani ya malalo takatifu ya Bibi Zainabu (a.s)”.

Akaendelea kusema “Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza yenye vipengele tofauti katika kukumbuka kifo cha Bibi Zainabu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: