Mawakibu za watu wa Karbala zinaomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeshuhudia mawakibu za watu wa Karbala zikija kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mawakibu za watu wa Karbala zimefanya matembezi ya kuomboleza kwa kuelekea katika malalo mbili takatifu, Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kurahisisha shughuli za uombolezaji.

Mmoja wa wahudumu wa mawakibu Sayyid Nizaar Hussein Abdu-Aun amesema “Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza msiba huu mbele ya malalo takatifu na kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufiwa na dada yao Bibi Zainabu (a.s), katika matembezi hayo wamebeba jeneza la kuigiza”.

Mmoja wa washiriki wa Maukibu Sayyid Ali Muhammad Karbalai amesema “Siku kama ya leo kila mwaka mawakibu kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, huja kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s), nakueleza utukufu wake, kujitolea kwake na namna alivyo fanyiwa dhulma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: