Ugeni wa Ataba nchini Sirya umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya uliopo Sirya, umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) mbele ya malalo yake takatifu jijini Damaskas.

Mjumbe wa ugeni huo Sayyid Murtadha Zaini amesema “Ugeni kutoka Ataba umefanya majlisi ya kuomboleza leo mchana ndani ya ukumbi wa haram ya Bibi Zainabu (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imehusisha usomaji wa ziara maalum ya Imamu Hussein (a.s) ya mwezi kumi na tano Rajabu, kisha akapanda kwenye mimbari muhadhiri Shekhe Abdullahi Dujaili, akafuatiwa na muimbaji Murtadha Harbu, majlisi imepata mahudhurio makubwa kutoka sehemu tofauti za nchi”.

Akaendelea kusema “Mzungumzaji ameeleza historia ya Bibi Zainabu (a.s) na jinsi alivyo pambana kunusuru harakati ya kaka yake Imamu Hussein (a.s), sambamba na kueleza mazingira magumu aliyopitia katika vita ya Twafu na baada ya vita hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: