Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.

Maukibu hiyo imeanzia ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikaelekea Atabatu Husseiniyya kwa kupitia uwanja wa katikati ya Ataba mbili huku wakiimba qaswida za kuomboleza.

Walipofika kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza iliyohudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru, qaswida na tenzi za kuomboleza zimeimbwa katika majlisi hiyo, sambamba na kueleza mitihani aliyopitia Bibi Zainabu (a.s) katika harakati za kumsaidia kaka yake na kulinda misingi ya Dini tukufu.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hufanya maukibu ya pamoja katika kila tukio la kuomboleza kifo cha mtukufu miongoni mwa Ahlulbait (a.s). katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: