Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake imetoa muhadhara kuhusu neema ya wilaya kwa Ahlulbait (a.s).

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muhadhara kuhusu neema ya wilaya kwa Ahlulbait (a.s).

Kiongozi wa idara bibi Adhraa shami amesema “Idara imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya kuzaliwa Imamu Ali (a.s) ndani ya Ataba tukufu, imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Hibatu Ridhwa, ikafuatiwa na muhadhara kuhusu neema ya wilaya ya Ahlulbait (a.s), uliotolewa na mmoja wa watumishi wa idara”.

Akaongeza kuwa “Hafla imeshuhudia shindano kwa mazuwaru na usomaji wa hadithi na sifa za bwana wa mawasii -a.s-” washiriki wa shindano hilo wamepewa zawadi za tabaruku kutoka kwenye haram tukufu, mmoja wa wasomaji wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya amesoma tenzi na dua ya Faraji ya Imamu wa zama (a.f)”.

Kuadhimisha mazazi haya kunalenga kutambulisha historia ya Imamu Ali (a.s), hakika yeye ni msingi wa maadili ya kibinaadamu yaliyohusiwa na Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: