Muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu nchini India amesema (Kongamano la kiongozi wa waumini -a.s) ni miongoni mwa makongamano makubwa zaidi hapa nchini.

Muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu nchini India Sayyid Ahmadi Al-Aabidi amesema kuwa, kongamano la kiongozi wa waumini (a.s) ni miongoni mwa makongamano makubwa hapa nchini hususan katika jiji la Mombai, jiji hili limejaa waislamu, wanakadiriwa idadi yao kufika milioni tatu.

Akasema “Tunatoa shukrani nyingi kwa ugeni kutoka Ataba tukufu, kwa kazi kubwa waliyofanya ya kufanikisha kongamano hili, tunatamani lifanyike kwenye miji mingine ya waislamu”.

Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano chini ya kauli mbiu isemayo (Kiongozi wa waumini -a.s- ni Haruna wa Uimamu na shahidi wa siku ya kiyama) kongamano hilo ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s) na limedumu kwa muda wa siku tatu, kwa ushiriki wa Ataba tofauti za Iraq.

Kongamano lilikuwa na vipengele tofauti, miongoni mwa vipengele hivyo ni kutembelea hauza na shule za kidini, kugawa zawadi za tabaruku, kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani na kupiga kura ambayo washindi wanapata zawadi ya Kwenda kufanya ziara katika Ataba tukufu za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: