Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea kufanya nadwa za Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya mkoani Karbala.
Wasimamizi wa nadwa hizo ni Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa, hukaribishwa wasomi wa Qur’ani tukufu kwa lengo la kujenga uwelewa wa Qur’ani katika Jamii.
Tawi la Maahadi katika wiki hii, limefanya nadwa iliyosimamiwa na haafidh wa Nahaju-Balagha Shekhe Haani Rabii, amebainisha nafasi ya Imamu Ali (a.s), akabainisha kauli yake isemayo “Aliniweka kwenye miguu yake nilipokuwa mdogo, akanikumbatia kwenye kifua chake”, maneno hayo yanamkusudia Mtume (s.a.w.w).
Nadwa imepambwa na usomaji wa Qur’ani kutoka kwa Muhammad Murtadha Aljaburi, mbele ya kundi kubwa la waumini waliohudhuria.