Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye maonyesho hayo kupitia matawi (21) ambayo ni mashirika na vitengo, yanaonyesha bidhaa za afya, elimu, viwandani, kilimo, vyakula, teknolojia na umeme.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria, wakuu wa vitengo na wasaidizi wao.
Maonyesho haya ya awamu ya tatu, jumla ya mashirika tofauti (26) ya viwanda, kilimo, biashara, afya, na elimu wameshiriki.
Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho haya, unalenga kuonyesha mafanikio ya Ataba katika sekta ya utoaji wa ajira katika jamii, mchango wake katika kukuza pato la taifa na kuonyesha namna inavyo ingiza bidhaa kwenye soko la taifa.