Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria amesema: Maonyesho yamefanyika kwa ajili ya kutambulisha jamii harakati na mafanikio ya Atabatu Abbasiyya.

Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami amesema kuwa, maonyesho ya tatu yamefanywa kwa lengo la kuonyesha jamii harakati zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ameyasema hayo alipotembelea maonyesho yanayo endelea katika chou kikuu cha Alkafeel.

Akasema kuwa “Uandaaji wa makumbusho ni jambo la kimazingira na husaidia kutambulisha harakati zinazofanywa na mashirika na vitengo vinavyo shiriki”.

Akaongeza kuwa “Maonyesho ya awamu ya tatu yanalenga kutambulisha jamii harakati na bidhaa zinazotengenezwa na Atabatu Abbasiyya za aina zote”.

Akasema kuwa “Uwepo wa wanafunzi kwenye maonyesho, itasaidia kuwatambulisha soko la kazi na watajikuta wapo mahala wanapotaka, aidha wasimamizi wa maonyesho watatambua uwezo wa wanafunzi na kuwapa nafasi za kazi”.

Akabainisha kuwa “Maonyesho yanalenga kueneza utamaduni na elimu, pamoja na lengo lake kuu la kutoa nafasi za kazi kwa wahitimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: