Kitengo cha Habari na utamaduni kinaomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) nchini Tanzania.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) katika nchi ya Tanzania barani Afrika.

Mkuu wa Markazi muheshimiwa Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema kuwa “Markazi imeomboleza kifo cha Aqilatu-Twalibina (a.s) katika bara la Afrika kupitia majlisi iliyofanywa nchini Tanzania”.

Akaongeza kuwa “Muwakilishi wa Markazi katika mkoa wa Kigoma nchini Tanzania Shekhe Ammaari Maulidi, amefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) iliyohudhuriwa na kundi kubwa la wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya harakati za kitablighi kielimu na kibinaadamu katika bara la Afrika kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya na wawakilishi wake waliopo katika nchi za Afrika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: