Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel imefanya mkutano wa kuweka mikakati ya mwaka 2024.

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mkutano wa kujadili mikakati na ratiba ya mwaka mpya.

Mkutano umejikita katika utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na idara kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kikao kimeangazia kwa kina namna ya kuhudumia kundi la vijana, kwa kuwapa malezi bora sambamba na misingi ya kiislamu na mwenendo wa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s), na njia za kufikisha mafundisho hayo kwenye mikoa mingine ya Iraq.

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel hufanya makumi ya ratiba za Skaut kwa mwaka, zinazolenga kutoa malezi bora kwa vijana na kukuza vipaji vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: