Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimepokea ugeni wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Alqadisiyya.
Mmoja wa watumishi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule chini ya kitengo Sayyid Amiri Haadi Jaliil amesema kuwa, “Watumishi wa kitengo cha mahusiano wamepokea ugeni wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Alqadisiyya”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa ratiba kamili inayohusisha mihadhara ya kidini, utamaduni, kutembelea Ataba mbili tukufu, Husseiniyya na Abbasiyya Pamoja na kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya, kikiwemo kiwanda cha Aljuud, kiwanda cha uchapaji wa vitabu Alkafeel na makumbusho ya Alkafeel”.
Rais wa ugeni huo Sayyid Hussein Azizi Dulaimi amesema “Wanafunzi wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya kwa kuwapa nafasi ya kushiriki katika ratiba hii inayohusisha karibu wanachuo (40)”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya hufanya ratiba za kuwajengea uwezo wadau wake katika mambo mbalimbali”.










