Walimu na wanafunzi wa Maahadi ya turathi chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi, wamepongeza kazi inayofanywa na kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya ya kutunza turathi na kufanya hakiki za kiislamu.
Ugeni huo unaongozwa na mkuu wa Maahadi ya turathi Sayyid Abdulhakim Swafi, wameangalia kazi zinazofanywa na kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi chini ya maktaba na Daru-Makhtutwaat, na mafanikio yake katika kuimarisha ushirikiano na kufanyia kazi mihadhara ya kielimu inayotolewa na kituo hicho.
Mkuu wa kituo Sayyid Swalahu Mahadi Abdulwahabu ameeleza kwa ufupi kuhusu kazi zinazofanywa na vitengo, aidha wageni wametembelea sehemu tofauti za kitengo hicho na kuangalia kazi zinazofanywa na miradi ya baadae.
Ugeni umepongeza kazi nzuri inayofanywa na kitengo ya kutunza na kuhakiki turathi za kiislamu sambamba na maendeleo makubwa ya teknolojia yanayotumika katika sekta hiyo.