Kitengo cha maarifa kimefanya kongamano la kitamaduni awamu ya kumi na nne katika mkoa wa Baabil.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya kongamano la kitamaduni awamu ya kumi na nne katika mkoa wa Baabil.

Mkuu wa kituo cha turathi za Hilla Shekhe Swadiq Khawilidi amesema “Kituo kimefanya kongamano la kumi na nne, imetolewa mihadhara miwili kutoka kwa Dokta Hashim Mussawi na Dokta Ali A’araji”.

Akabainisha kuwa “Muhadhara wa kwanza ulikuwa na anuani isemayo (Kujizuwia kwa Ibun Sukuun Alhilliy katika nukuu za Nahajul-Balagha – utafiti katika tofauti za dalili) kutoka kwa Dokta Mussawi, akabainisha juhudi za Ibun Sukuun Alhilliy katika Nahajul-Balagha, muhadhara wa pili ulikuwa na anuani isemayo (Hakiki zilizopita kuhusu Nahajul-Balagha) kutorejea katika nakala zilizoandikwa katika mji wa Hillah (Ameeleza hakiki zilizopita za kitabu cha Nahajul-Balagha, zilizofanywa na wanachuoni wakubwa wa uhakiki na kuchapishwa na wanachuoni wa Hilla”.

Akaendelea kusema “Kongamano limehudhuriwa na wasomi na wabobezi wa mambo hayo, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kutunza turathi katika kizazi cha sasa na vijana wenye kujitambua”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: