Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha nane cha ratiba ya malezi ya Skaut.
Ratiba imefunguliwa kwa kupandisha bendera ya Iraq na kusoma Qur’ani, iliyofuatiwa na kubainishwa mafundisho muhimu kwa wahudumu wa kujitolea katika program za Skaut.
Ratiba imepambwa na warsha za kimalezi, mihadhara, uboreshaji wa vipaji vinavyosaidia kujenga heshima ya mtu na kuimarisha misingi ya ubinaadamu na uislamu.
Ratiba hii ni sehemu ya kutumia vizuri msimu wa likizo na kutambua vipaji vya wanaskaut pamoja na kuviendeleza na kuwaelekeza katika njia sahihi.