Taasisi ya Waafi ya utafiti na utunzaji wa vielelezo katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha warsha ya utunzaji wa picha na vielelezo kwa watumishi wa taasisi ya Shuhadaa.
Rais wa taasisi Muhandisi Ahmadi Swadiq amesema “Warsha ya kimasomo imefanywa kwa watumishi wa taasisi ya Shuhadaa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutunza picha za vielelezo chini ya utaratibu Madhubuti kwa lengo la kutumikia jamii”.
Akaongeza kuwa “Elimu ya kutunza vielelezo ni muhimu sana kwa vizazi vijavyo na kutunza urithi wa kihistoria kwa taifa”.
Akasisitiza kuwa “Kuna elimu inayosaidia kutunza vielelezo na vitu muhimu kwa watafiti na wanahistoria, sambamba na kutunza taarifa muhimu na kuhakikisha hazipotei na hazisahauliki, jambo ambalo linasaidia watu kusoma mambo ya zamani”.