Majmaa-Ilmi yahitimisha ratiba ya Qur’ani katika mkoa wa Waasit.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha ratiba ya vituo vya Qur’ani katika mtaa wa Dabuni kaskazini ya mkoa wa Waasit.

Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa, imeweka vituo vitano katika mtaa wa Dabuni kwa ushiriki wa walimu (15) waliokuwa wakifundisha na kusahihisha usomaji wa surat Fat-ha na sura zingine fupi Pamoja na nyeradi za swala na kujibu maswali yanayohusu Qur’ani.

Hali kadhalika Maahadi ilituma mubalighina kwa ajili ya kujibu maswali ya kisheria na kutoa mihadhara kwa mazuwaru watukufu, Pamoja na kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani, majlisi za kuomboleza, kuongoza swala za jamaa na kutabaruku kwa bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Watumishi wa Majmaa wameenda mji mkuu wa Baghdad kukamilisha ratiba katika mji mtukufu wa Kadhimiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: