Majmaa-Ilmi imeandaa mahafali ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeandaa mahafali ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa kupitia ratiba ya mahafali zake za kila wiki za (Arshu-Tilaawah).

Kiongozi wa kamati tendaji Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi amesema “Markazi imeandaa mahafali ya usomaji wa Qur’ani ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, chini ya kituo cha miradi ya Qur’ani na kupitia ratiba ya mahafali za usomaji wa Qur’ani za kila wiki (Arshu-Tilaawah)”.

Akaongeza kuwa “Mahafali za usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya kunufaika na mihadhara ya kidini na kiibada sambamba na usomaji maalum wa Qur’ani kutoka kwa wanafunzi wa mradi, wataendelea kufanya hivyo pia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Mahafali inalenga kukusanya wasomaji wenye vipaji kwa ajili ya kubadilishana uzowefu na kuinua viwango vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: