Ameyasema hayo alipompokea muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Sanad nchini Pakistan Shekhe Muhammad Muhsin Almahdawi, na kusikiliza maelezo kuhusu hali ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kijamii, kiuchumi na kielimu katika taifa hilo.
Sayyid Swafi ameeleza historia ya kufika Dini ya kiislamu katika miji hiyo na namna ilivyo sambaa.
Akasisitiza umuhimu wa kujenga mahusiano mazuri na watu wa Dini zingine na kuonyesha picha nzuri ya madhehebu ya Ahlulbait (a.s).
Amehimiza kujali masomo ya Dini na shule za Dini zilizopo katika mji huo samamba na kujali masomo ya kisekula, akatoa wito wa kudumisha maadhimisho ya Husseiniyya na kuwakumbuka Maimamu wa Ahlulbait (a.s).
Shekhe Muhammad Muhsin Almahdawi amesema “Nimefanikiwa kutembelea Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi”.
Akaongeza kuwa, hakika Sayyid Swafi anajua mambo mengi kuhusu historia ya mji wa Sanad na Pakistani kwa ujumla, ameonyesha kufurahishwa sana na ziara hii pamoja na nasaha alizopewa na Sayyid Swafi.