Makumbusho ya Alkafeel imesema: mamia ya mazuwaru wanaingia kila siku kuangalia mali-kale zilizopo ndani ya makumbusho.

Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya hupokea mamia ya mazuwaru kila siku wanaokuja kuangalia mali-kale.

Rais wa kitengo cha makumbusho Sayyid Swadiq Laazim amesema “Kitengo cha makumbusho hupokea mamia ya mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku, ambao huja kuangalia mali-kale zilizopo ndani ya makumbusho ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Milango ya makumbusho hufunguliwa kila siku kwa muda wa saa (12) kuanzia saa (3) asubuhi hadi saa (3) usiku, wakati wa swala milango hufungwa na hufunguliwa baada ya swala ya jamaa”.

Akaendelea kusema “Makumbusho inafanya kazi kubwa ya kutambulisha historia ya Ataba tukufu kwa kizazi cha sasa na kuonyesha hatua tofauti ambazo Ataba ilipitia, sambamba na kuonyesha vielelezo halisi vya shambulio lililofanywa na utawala uliopita katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: