Kamati ya maandalizi imekamilisha ratiba ya wiki.

Kamati ya maandalizi katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha ratiba ya wiki kwa watumishi wa Ataba tukufu.

Ratiba imesimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, ilikuwa na vipengele vya kidini, kitamaduni, warsha za kujenga uwezo, mashindano tofauti pamoja na kutembelea miradi ya Ataba tukufu.

Ratiba inalenga kudumisha mawasiliano baina ya watumishi na kuwaonyesha harakati za Ataba tukufu katika sekta ya elimu, viwanda, kilimo, malezi pamoja na mambo ya kitamaduni.

Hafla ya kufunga ratiba hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Mahadi (a.f), ambapo rais wa kitengo cha uboreshaji Dokta Muhammad Hassan Jaabir ametoa nasaha muhimu kwa washiriki, ratiba ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi washindi wa mashindano matatu yaliyofanywa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: