Kituo cha utamaduni wa familia kimeandaa programu ya walezi wa shule za awali (chekechea) za Al-Ameed.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba maalumu kwa walezi wa shule za awali za Al-Ameed kwa anuani isemayo “Walezi wa mwezi”.

Mkuu wa kituo cha utamaduni wa familia bibi Sara Alhafaar amesema, “Programu imeshuhudia muhadhara kuhusu namna ya kuwasiliana na watoto kutoka kwa mlezi Nabaa Swabaah Alhaidary”.

Katika programu hiyo kulikuwa na kipengele cha mashindano ya kielimu kutoka kwa mlezi Kawakibu Abdusataar.

Kituo kinafanya kila kiwezalo kujenga uwezo wa walezi kwa lengo la kuboresha malezi ya watoto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: