Ameyasema hayo alipokutana na mkuu wa kituo cha picha na katuni Aljuud chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Twalibu Abdul-Amiir, baada ya kusikiliza maelezo ya kina kuhusu harakati za kituo na kazi ya mwisho waliyofanya ya filamu ya (Thulatiyyatul-Maa).
Akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya imekuwa ikisaidia kukuza vipaji tofauti, pia kuna mambo mengi ya kihistoria yanayoweza kutumika katika sekta hiyo.
Akahimiza watumishi wa kituo cha utengenezaji wa filamu kutumia historia za Mitume na Maimamu wa Ahlulbait (a.s) zenye uwezo mkubwa wa kurekebisha tabia za vijana na kuwafanya kuwa na maadili mema.
Akahimiza kutumia lugha nzuri katika utengenezaji wa filamu na taarifa sahihi zinazoendana na misingi ya sheria.
Sayyid Ahmadi Twalibu akasema, Leo nimefanikiwa kukutana na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya na kumuambia kazi zinazofanywa na kituo cha picha na katuni ikiwemo filamu ya (Thulathiyyatul-Maa).
Muheshimiwa amepongeza kazi zinazofanywa na kituo chetu hasa uandaaji wa filamu ya (Thulathiyyatul-Maa) na ametupa ushauri wa namna ya kupanua utendaji wetu.