Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Abduswahibu Twaiy amesema, “Majlisi hiyo ni sehemu ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) na itadumu kwa muda wa siku tatu, idara huhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) ikiwa ni pamoja na kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s)”.

Akaongeza “Muhadhiri wa Majlisi Shekhe Murtadha Alkhafaaji ameongea kuhusu historia ya Imamu Alkaadhim (a.s) na njia aliyotumia kupambana na vikra potofu wakati wake sambamba na sehemu ya Maisha yake (a.s) ya kiibada”.

Akabainisha kuwa “Muhadhara umeelezea dhulma alizofanyiwa Imamu Alkaadhim (a.s) na watawala za zama zake hadi walivyo mkamata na kumfunga kwenye jela zenye giza”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: