Watumishi wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wamekamilisha maandalizi ya ratiba ya (Qur’ani ndogo) katika kitongoji cha Kadhimiyya jijini Baghdad.
Ratiba hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa-Ilmi, kwa lengo la kujenga uwelewa kwa mazuwaru wanaokuja kushiriki maombolezo ya kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s).
Ratiba inahusisha vipengele vingi, kuna mashindano ya Qur’ani, michezo ya kielimu, michoro na swala ya jamaa baada ya mihadhara elekezi.