Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim katika ukumbi wa utawala.
Kiongozi wa idara ya kupokea wageni katika ukumbi wa utawala Sayyid Faarisi Husseini amesema “Tumefanya Majlisi kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, chini ya uhadhiri wa Shekhe Muzharu Almansuuri ambae ameongea kuhusu maisha ya Imamu Alkaadhim (a.s) na yaliyojiri dhidi yake”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imehudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa Ataba tukufu, watumishi na wageni, itaendelea kwa muda wa siku mbili”.
Atabatu Abbasiyya tukufu hutilia umuhimu maalum katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kufikisha ujumbe wao na kufuata mwenendo wao mtukufu.