Atabatu Abbasiyya tukufu imepandisha bendera ya Imamu Alkaadhim (a.s) katika kuomboleza kifo chake, kwenye uwanja wa Qubla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Viongozi kadhaa wa Atabatu Abbasiyya wameshuhudia tukio hilo pamoja na kundi la mazuwaru na waumini, rais wa kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Ataba tukufu ikiwemo Atabatu Abbasiyya zimezowea kupandisha bendera ya huzuni katika kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s) kama alama ya kuingia kwa kipindi cha huzuni”.
Akaongeza kuwa “Tukio la kupandisha bendera limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na Majlisi iliyohudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) waliokuja kuomboleza msiba huo”.
Shughuli ilikuwa na vipengele vingi vya uombolezaji, ikiwa ni Pamoja na muhadhara ulioeleza dhulma alizofanyiwa Imamu Alkaadhim (a.s) na msimamo wake dhidi ya mtawala dhwalimu.