Mawakibu za watu wa Karbala zinaomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s).

Mawakibu za watu wa Karbala zimeomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Mawakibu za watu wa Karbala zimefanya matembezi ya kuomboleza asubuhi ya Jumanne, zikaelekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakipitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Waombolezaji wamebeba jeneza la kuigiza kama jeneza la Imamu Alkaadhim (a.s), kulikuwa pia na waombolezaji wapiga zanjiil walioimba qaswida na tenzi mbalimbali kuhusu msiba huo, katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi kwa waombolezaji na mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: