Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) kupitia maukibu ya Pamoja.
Maukibu imeanza matembezi yake ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kusimama kwa mistari, kisha wakaelekea katika malalo ya mwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba qaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Matembezi yakaishia ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza, kwa ushiriki wa watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kundi kubwa la mazuwaru.
Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, hufanya maukibu ya pamoja katika kila tukio la kuomboleza kifo cha Ahlulbait (a.s) wakati wote wa mwaka.