Sayyid Swafi amekagua kazi zinazofanywa na taasisi ya Utafiti na Uhakiki Alwaafi.

Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amekagua kazi zinazofanywa na taasisi ya Utafiti na Uhakiki Alwaafi.

Rais wa taasisi hiyo, Sayyid Ahmadi Swadiq amesema “Sayyid Swafi ameangalia kazi zilizofanywa na taasisi ya Alwaafi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu toka kuanzishwa kwake, na wapi imefika baadhi ya miradi yake”.

Akaongeza kuwa “Ziara hii ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu wa kutembelea vitengo vya Ataba na kuangalia utendaji wake”.

Akaendelea kusema “Sayyid Swafi amesikiliza maelezo kuhusu miradi inayofanywa na taasisi na mafanikio yake, kwa mfano mradi wa kitabu cha Fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda, kitabu cha wafungwa wa kisiasa, kitabu cha Marjaiyya Diniyya na vinginevyo, Pamoja na kazi zingine zinazohusu historia ya Iraq ya sasa na zamani”

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa tasisi ya Alwaafi amesema kuwa, miongoni mwa mambo aliyo angalia Muheshimiwa Sayyid Swafi ni filamu za mashahidi wa fatwa tukufu, baadhi ya miradi, mtandao wa kielektronik, amekutana na watumishi wa taasisi na kusikiliza mahitaji yao na mafanikio yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: