Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inafanya semina ya hukumu za Fiqhi kwa vijana.

Jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya hukumu za Fiqhi kwa vijana.

Mkufunzi wa semina hiyo Shekhe Yunusi Ashuur amesema kuwa, semina ilikuwa na washiriki (150), wamefundishwa hukumu za fiqhi zinazohusiana na adabu ya Adhana na umuhimu wake katika Dini ya kiislamu.

Semina hii ni sehemu ya ratiba ya kukuza elimu ya Dini kwa wanaskaut na kuwashajihisha kushiriki katika mambo ya kijamii.

Nayo ni kielelezo tosha namna ya Jumuiya ya Skaut inavyojali mafundisho ya Dini katika jamii sambamba na kuwajengea vijana msingi mzuri wa masomo ya Dini.

Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel huandaa ratiba tofauti za kielimu na kitamaduni, kwa lengo la kudumisha muingiliano wa kijamii na kuimarisha utamaduni wa kushikamana na mafundisho ya Dini katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: