Majmaa-Ilmi imefanya semina ya usomaji wa Qur’ani.

Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya semina ya Qur’ani iliyojikita katika (matamshi na sifa za herufi).

Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani mjini Najafu Sayyid Ahmadi Zamili amesema “Semina ni sehemu ya mkakati wetu wa elimu wa mwaka (2024) katika mkoa wa Najafu na wilaya zake, itaendelea kwa muda wa siku (45) kila wiku kutakua na mihadhara miwili”.

Akaongeza kuwa “Semina inalenga kuibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani na kuandaa walimu watakaochukua jukumu la kufundisha Qur’ani katika miji yao na kushiriki kwenye mashindano ya Qur’ani”.

Akaendelea kusema “Mkufunzi wa semina hiyo ni Ustadhi Aadil Yasiri na inawashiriki (50), wanafundishwa kwa nadhariyya na vitengo, wanafundishwa aina za sauti za kiarabu, matamsi ya herufi, sifa za herufi, hukumu za usoaji na kutambua makosa yanayofanywa na wasomaji wengi ya Qur’ani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: