Majlisi ya wanachuoni wa muungano wa Muhammadiy wamesema: Kongamano la Nabiyyu-Rahmah ni wito wa kuondoa ubaguzi katika jamii.

Mjumbe wa Majlisi ya wanachuoni wa muungano wa Muhammadiy katika mji wa Nainawa Sayyid Ahmadi Idrisa amesema kuwa, kongamano la Nabiyyu-Rahmah (s.a.w.w) linalingania amani na kuondoa chuki katika jamii.

Yamesemwa hayo katika shughuli za ufunguzi wa kongamano la Nabiyyu-Rahmah (s.a.w.w) awamu ya pili, linalosimamiwa na kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya chini ya idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel katika chuo kikuu cha Mosul.

Idrisa akasema “Kongamano ni miongoni mwa mambo mazuri yanayofanywa na Ataba tukufu, linahusisha jamii zote za watu wa Iraq na kuwa mfano mwema unao onyesha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni rehema kwa walimwengu wote”.

Akaongeza kuwa “Kongamano linalingania amani na kukemea ubaguzi katika jamii sambamba na kuwataka watu kutambua itikadi sahihi ya kiislamu na mwenendo wa Mtume wetu na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Pembezoni mwa kongamano hilo yamefunguliwa maonyesho ya vitabu na picha kwa ushiriki vitengo tofauti vya Ataba tukufu, kama vile kitengo cha Habari na utamaduni, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, mali-kale kutoka kwenye makumbusho ya Alkafeel Pamoja na ushiriki wa maktaba kuu ya chuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: