Kupitia program ya (Ulizeni wanaojua) Idara ya Fatuma bint Asadi imehuwisha siku ya (Mab’ath) kupewa Utume.

Idara ya Fatuma bint Asadi katika Atabatu Abbasiyya, imehuisha siku ya (Mab’ath) kupewaUtume kwa kufanya hafla ndani ya ratiba yake ya wiki ijulikanayo kwa jina la (Ulizeni wanaojua).

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, mbele ya kundi kubwa la mazuwaru, ukafuata muhadhara kutoka kwa muhadhiri wa Husseiniyya, ameongea kuhusu kupewa Utume na tofauti baina yake na safari ya Israa na Miraji.

Imeshiriki maktaba ya Ummul-Banina (a.s) katika hafla hiyo, kwa kufanya shindano lililojikita katika kuuliza maswali yanayohusu kupewa Utume, kisha wakagawa zawadi kwa washindi.

Hafla imepambwa na ratiba ya (Uwanja wa Watoto) karibu watoto hamsini wameshiriki kwenye ratiba hiyo, ambapo wamefanya shindano maalum linalohusu kupewa Utume (Mab’ath) na washindi wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: