Sayyid Swafi amesema: Sekta ya sekula ni muhimu na inanafasi kubwa katika kujenga jamii na inapasa kuisapoti.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, sekta ya sekula ni muhimu na inamchango mkubwa katika kujenga jamii na inapasa kuisapoti.

Ameyasema hayo wakati akimpokea kiongozi wa maafisa elimu katika mkoa wa Karbala Dokta Muniir Daaimi na wajumbe aliofuatana nao, baada ya kusikiliza maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na maafisa elimu katika jamii ya wasomi hapa mkoani.

Muheshimiwa Sayyid Swafi akataja msaada unaotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye sekta ya elimu za kisekula, Ataba inatumia njia tofauti kusaidia sekta hiyo, akafafanua kuwa “Sekta ya sekula ni muhimu na inamchango mkubwa yatupasa kuisapoti”.

Akasisitiza kuwa afisa elimu anatakiwa awe na elimu itakayomuwezesha kusimamia na kuelekeza fikra za mwanafunzi pamoja na kutatua changamoto zake, sambamba na kulinda misingi ya kiislamu na kuifundisha kwa wanafunzi.

Kwa upande wa Daaimi amesema, ujumbe wa maafisa elimu umekutana na Sayyid Swafi na kuongea mambo mengi yanayohusu elimu na taasisi za kisekula, akaongeza kuwa Sayyid Swafi amesisitiza kusaidiwa sekta hii kutokana na huduma kubwa inayotolewa katika jamii.

Akaongeza kuwa, tumesha kagua kiwango cha elimu kinachotolewa na vyuo vikuu vilivyo chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, sisi katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu tunajivunia mafanikio ya vyuo vikuu vya Ataba na nafasi za juu walizopata za ubora, hakika kuna mazingira bora ya elimu, majengo, vifaa bora vya kufundishia, mambo hayo yana athari kubwa kwa kuvutia wanafunzi, pamoja na kiwango cha juu kabisa cha elimu, malezi na maadili katika taasisi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: