Waziri wa elimu ya juu amempa zawadi mkuu wa kitivo cha afya na udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel.

Waziri wa elimu ya juu na tafiti za kielimu Dokta Naiim Abudi, amempa zawadi mkuu wa kitivo cha afya na udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Fadhili Ismail Twaaiy.

Hafla ilikuwa ya kutoa zawadi kwa walioshinda zawadi ya chuo cha Ain awamu ya nne mwaka 2024, zawadi ilihushisha watafiti waliofanya vizuri, walioshika nafasi za kwanza katika vyuo vikuu, wenye tafiti zenye athari kubwa na waandishi wa vitabu.

Twaaiy amepokea zawadi katika hafla ya watafiti na waliopata nafasi za kwanza kwenye vyuo vikuu katika mambo ya tafiti za kielimu, ameonyesha kufurahi sana kwa kupata zawadi hiyo, akaonyesha umuhimu wa tafiti za kielimu katika kuendeleza jamii na kuinua kiwango cha elimu.

Zawadi hiyo inatokana na kazi kubwa anayofanya mkuu wa kitivo, ya kuinua kiwango cha tafiti za kielimu sambamba na jinsi chuo kinavyojali kuendeleza sekta ya afya na udaktari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: