Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ameangalia kazi zinazofanywa na kituo cha turathi za Hilla

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini ameangalia kazi zinazofanywa na kituo cha turathi za Hilla katika mkoa wa Baabil.

Muheshimiwa katibu mkuu na msaidizi wake Muhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, wametembelea kituo kilichochini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kuangalia utendaji wa kazi na kuangalia mafanikio na mahitaji.

Ugeni umepokewa na mkuu wa kituo Shekhe Swadiq Khawilidi, akatoa maeleza kuhusu kazi zinazofanywa na kituo na mikakati ya baadae, akasema watumishi wa kituo wanaendelea kuhakiki vitabu, kuandika vitambu mbalimbali, kufanya semina za kujenga uwezo na kufanya nadwa kwa ajili ya kuhuisha turathi za kiislamu katika mji wa Hilla.

Muheshimiwa katibu mkuu wakapongeza kazi nzuri inayofanywa na kituo ya kuhuisha turathi za kiislamu, akasisitiza umuhimu wa kuendelea kutunza mafanikio hayo.

Hiyo ni sehemu ya ziara zinazofanywa na uongozi mkuu wa Ataba kwa ajili ya kuangalia utendaji na kutatua changamoto kwenye vitengo, idara na vituo vilivyo chini yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: