Majmaa-Ilmi imefanya semina ya kwanza ya Usulu na Manaahiju-Tafsiri katika mji wa Najafu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, imefanya semina ya Usulu na Manaahiju-Tafsiri kwa mara ya kwanza.

Mjumbe wa idara ya mambo ya hauza katika Maahadi Shekhe Wasam Sabyi amesema “Semina imefanywa katika shule ya marehemu Marjaa-Dini Sayyid Muhsin Hakiim kwa ushiriki wa wanafunzi (20), mkufunzi wa semina hiyo alikuwa ni Shekhe Muhsin Jaswani, amefundisha mitazamo ya msingi katika Manaahiju-Tafsiri”.

Akaongeza kuwa “Semina hii ni sehemu ya ratiba ya masomo ya Qur’ani, chini ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini unaosimamiwa na Majmaa-Ilmi kwa wanafunzi wa hauza katika mji wa Najafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: