Kitengo cha Habari na utamaduni kimetangaza kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza kufanya kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya katika viwanja vya ukanda wa kijani.

Kiongozi wa jumuiya ya Skaut ya Alkafeel Sayyid Ali Hussein amesema kuwa “Kongamano linafanywa sambamba na kuingia mwezi mtukufu wa Shabani, litakuwa na vipengele tofauti.

Akaongeza kuwa “Kutakuwa na igizo litakalo onyesha matukio muhimu katika Maisha ya Ahlulbait (a.s) pamoja na qaswida za kidini, mashindano ya kitamaduni na kidini, michezo na mambo mengine yanayosaidia kukuza fikra na uwelewa wa mtoto”.

Kongamano litafanywa katika viwanja vya ukanda wa kijani, kwenye uwanja wa Rasulul-Akram (s.a.w.w), uliopo nyuma ya hospitali ya Imamu Hassan (a.s) siku ya Jumanne na Jumatano, sawa na tarehe (13 -14 – Februali 2024m saa moja jioni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: