Jumuiya ya Al-Ameed imetafsiri jarida la kumbukumbu ya Samaraa kwa picha.

Jumuiya ya kielimu Al-Ameed, kupitia rais wa kitengo cha tafsiri Dokta Haidari Ghazi Mussawi amesema kuwa tumefasiri jarida la (Kumbukumbu ya Samaraa) kwa picha.

Chapisho hilo limeonyesha picha za kihistoria katika zama tofauti za mji wa Samaraa, zinaonyesha kiwango cha utamaduni katika mji huo na mafundisho ya Dini, kama vile Atabatu Askariyya yenye malalo ya Maimamu wawili Askariyyaini (a.s) sambamba na thamani ya mali-kale na turathi.

Kitabu hiki cha picha kilicho tafsiriwa kwa lugha ya kiingereza na kituo cha turathi za Samaraa, ni kitabu muhimu kinacho onyesha picha halisi ya mji huo na kutambulisha kila kitu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: