Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza majina ya washindi wa shindano la kitamaduni lililofanywa kufuatia kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s).
Sharti la kupokea zawadi mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla itakayofanyika katika eneo la mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumanne (13/02/2024m) sawa na (2 Shabani 1445h) baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa kufika kwenye kitengo cha wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi siku nne toka kutangazwa kwa matokeo hayo, akiwa na kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria.
Shindano lilikuwa na washiriki (3395), idadi ya majibu sahihi (2484), majibu yasiokua sahihi (911), idadi ya washindi (10).