Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la kuonyesha mafanikio ya vitengo vyake

Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la kwanza kwa ajili ya kuangalia mafanikio ya vitengo vyake, kwenye ushiriki wa siku ya majukumu ya kitaifa.

Mjumbe wa kamati iliyoundwa kwa ajili ya kufatilia ripoti za vitengo Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umeunda kamati ya kufatilia ripoti za visa vya mafanikio, vilivyofanywa na vitengo vya Ataba tukufu na taasisi zilizochini yake, kuanzia kiwango cha utendaji wa mtu binafsi, kikosi au mradi kwenye ushiriki wa siku ya majukumu ya kitaifa inayosimamiwa na ofisi ya Waziri mkuu”.

Akaongeza kuwa “kongamano limehudhuriwa na viongozi wa Ataba kutoka sekta tofauti, kwa lengo la kujadili visa vyenye mafanikio kupitia mtu binafsi, kikundi au taasisi zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya katika sekta tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: